Baada ya Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuteuliwa kuwa Mlezi Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, mlinda mlango wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda, ametoa lake la moyoni juu ya uteuzi huo.
Kwa mujibu wa Radio One, Mapunda ambaye aliwahi kung'ara akiwa na Yanga, amesema kuwa maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumteua Mengi ni ya kufurahisha.
Kipa huyo wa zamani anaamini Mengi ataleta mchango mkubwa katika soka la Tanzania kutokana na kuwa sehemu ya soka kama mdau.
Aidha, Mapunda amesema Mengi si mgeni katika kujitoa kwa ajili ya kulisaidia soka la Tanzania kwani aliwahi pia kipindi kile wakati akiwa anaichezea Taifa Stars kipindi cha Marcio Maximo akiwa Kocha Mkuu.
Mbali na kuichezea Yanga, Mapunda aliwahi kuitumikia pia klabu ya Simba ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Bara baada ya kutwaa kikombe msimu wa 2017/18.
No comments:
Post a Comment